Nataja mambo ambayo huenda yakawa ni tatizo: je, inasihi au haisihi na kukubaliwa hajj ya ambaye haswali? Hapana. Kwa nini? Kwa sababu sio muislamu. Isitoshe haijuzu kumwacha ambaye haswali kuvuka mipaka ya Makkah. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا

”Enyi walioamini! Hakika washirikiana ni najisi, hivyo basi wasikaribie al-Masjid al-Haraam baada ya mwaka wao huu.”[1]

Wale ambao wanaishi pamoja na asiyeswali katika chumba kimoja basi wanalazimika kumwambia asilimu na vinginevyo watamzuia kuvuka mipaka ya Makkah.

[1] 09:28

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binothaimeen.net/content/17549
  • Imechapishwa: 26/07/2020