Swali: Kinajuzu kichinjwa cha mwanamke katika hali ya amechinja mbali na wanamme na kinaliwa?

Jibu: Kichinjwa cha mwanamke ni halali. Ni mamoja amefanya hivo mbele au mbali na wanamme muda wa kuwa ameteremsha damu na kutaja jina Allaah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Kuleni kile ambacho kimetolewa damu na kutajiwa jina la Allaah.”

Hakuna tofauti kati ya kwamba ni mwanamke huyo ni mwenye hedhi au msafi. Kwa sababu inafaa kwa mwenye hedhi kumtaja Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (2/20)
  • Imechapishwa: 26/07/2020