Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia mkono wa kushoto katika kuchinja au kuandika Qur-aan?

Jibu: Ndio, inafaa kwa mtu kutumia mkono wake wa kushoto katika kuchinja, kuandika Qur-aan na mambo mengine ikiwa ndio uwezo wake. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

”Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[1]

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[2]

[1] 02:286

[2] 64:16

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (2/20)
  • Imechapishwa: 26/07/2020