Swali: Ni kweli kwamba yule mwenye kuchinja Udhhiyah yake kabla ya kichinjwa cha imamu basi kichinjwa chake hakisihi?

Jibu: Sahihi ni kwamba yule mwenye kuchinja baada ya kumalizika swalah ya ´iyd basi kichinjwa chake kinasihi japo atakuwa amechinja kabla ya imamu. Kuhusu aliyechinja Udhhiyah yake kabla kuswaliwa swalah ya ´iyd hakisihi. Si vyenginevyo hicho ni chakula amewaharakishia familia yake.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah al-Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5123)
  • Imechapishwa: 26/07/2020