Hekima ya kurefushwa swalah ya usiku katika Ramadhaan

Swali: Ni ipi hekima baadhi ya Rak´ah katika kumi la mwisho la Ramadhaan ni ndefu katika kisomo chake, Rukuu´ zake na Sujuud zake na Rak´ah nyenginezo ni fupi?

Jibu: Kutokana na ninavyojua hakuna Sunnah Swahiyh inayojulisha juu ya hilo kwa upambanuzi. Lakini watu wamezowea hivo kwa ajili ya kuwakhafifishia watu na kuwapendezeshea kusimamisha swalah ya usiku. Atakayekhafifisha au akarefusha sehemu ya mwanzo ya usiku au mwishoni mwake hapana vibaya, pamoja na kuzingatia kuweka wazi kisomo, kuwa na unyenyekevu ndani yake na kuwa na utulivu ndani ya swalah na kutofanya haraka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/20354/بيان-الحكمة-في-اطالة-صلاة-القيام-في-رمضان
  • Imechapishwa: 19/03/2023