Ramadhaan kwa ambaye figo yake imefeli

Swali: Kuna mmoja figo lake limefeli na umri wake ni zaidi ya sabini. Baadaye aliwekwa figo moja na nyingine ikafeli. Madaktari wamemkataza kufunga.

Jibu: Alishe masikini nusu pishi kwa kila siku moja atakayokula.

Swali: Na Ramadhaan?

Jibu: Vivyo hivyo. Ikiwa si muweza wakithibitisha asifunge maishani basi awalishe masikini kwa kila siku moja nusu pishi.

Swali: Ngapi?

Jibu: Kila siku nusu pishi ambayo ni 1,5 kg ya tende, mchele au ngano.

Swali: Kila siku?

Jibu: Si lazima kufanya kila siku. Anaweza kuikusanya yote na akawapa nayo baadhi ya mafukara kwa muda wa mwezi mzima.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21409/حكم-من-عجز-عن-صوم-رمضان-للمرض
  • Imechapishwa: 19/03/2023