Bora swali na imamu Tarawiyh mpaka mwisho

Swali: Katika swalah ya Tarawiyh na baada ya imamu kuswali Witr na wakati imamu anatoa Tasliym hatutoi Tasliym pamoja naye bali tunasimama na kuswali Rak´ah ya nyongeza ili isiwe Witr. Tunafanya hivo kwa sababu tunataka kuchelewesha Witr mpaka baada ya kulala. Ni lipi bora; kumfuata imamu au kuchelewesha Witr?

Jibu: Jambo ni lenye wasaa. Yule mwenye kumfuata imamu ndiye bora. Aswali pamoja na imamu mpaka mwisho ili apate ujira kama yeye. Na ambaye ataswali Rak´ah nyingine moja na akaifanya shufwa witiri yake ili aswali Witr mwishoni mwa usiku, jambo ni lenye wasaa. Ingawa akitoa salamu pamoja naye ndio bora zaidi – Allaah akitaka. Baada ya hapo ataswali kile atachojaaliwa pasi na kuswali Witr. Ataswali Rak´ah mbili, Rak´ah nne, Rak´ah nane au zaidi ya hapo ambapo atatoa Tasliym kila baada ya Rak´ah mbili. Katika hali hiyo hakuna haja ya Witr. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna Witr mbili katika usiku mmoja.”

Lakini ataswali kile atachojaaliwa ambapo atatoa salamu baada ya Rak´ah mbili. Ingawa kama tulivosema bora ni yeye kutoa salamu pamoja na imamu na kunamtenga mbali na jambo la kujionyesha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11834/هل-الافضل-السلام-مع-الامام-حتى-ينصرف-في-قيام-رمضان
  • Imechapishwa: 19/03/2023