Ameacha kufunga baada ya baleghe kutokana na ujinga

Swali: Takriban miaka kumi iliyopita baleghe yangu ilipita kutokana na zile alama zinazojulikana za kubaleghe. Hata hivyo katika mwaka wangu wa kwanza wa baleghe yangu nilikutana na Ramadhaan na sikufunga pasi na udhuru unaokubalika katika Shari´ah. Hilo lilitokana na ujinga wangu katika kipindi hicho. Je, hivi sasa nalazimika kulipa? Je, mbali na kulipa, nalazimika kutoa kafara?

Jibu: Unalazimika kulipa mwezi huo ambao haukufunga pamoja na kutubu na kuomba msamaha. Mbali na hayo ni lazima pia kulisha masikini kwa kila siku moja kwa kiwango cha nusu pishi katika chakula kinacholiwa sana katika mji kama vile tende, mchele au vyenginevyo ikiwa unaweza kufanya hivo. Lakini ukiwa ni masikini na huna uwezo hakuna kinachokulazimu isipokuwa kufunga tu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/335)
  • Imechapishwa: 19/03/2023