Swali: Tunaomba ufafanuzi wa Hadiyth hii:
“Mwanamke yeyote ambaye atamuomba mume wake talaka bila ya sababu, basi ni haramu juu yake harufu ya Pepo.”
Jibu: Ufafanuzi ni kuwa, mwanamke asli yake ni mpungufu wa akili na dini. Kutokana na hili ndio Allaah akaifanya talaka kuwa kwenye mikono ya mwanaume. Vinginevyo, kila wakati mume anapomuudhi angemuomba mwanamke waachane. Lau Allaah angeiweka talaka kwenye mikono ya wanawake, basi mwanamke angelikuwa anamtaliki mume wake kwa siku mara ishirini. Allaahu ndiye mwenye kutakwa msaada. Mwanamke ni mpungufu wa akili na Dini kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akimuomba mume wake talaka na hakumfanyia jambo lolote baya, basi mwanamke huyo hatonusa harufu ya Pepo. Ama ikiwa mume anamfanyia mabaya, au mke akawa anamchukia na hawezi kumtekelezea haki zake, hapo anaweza kumuomba talaka. Ama ikiwa mume anamfanyia mabaya. Hakika Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُوا حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَا إِن يُرِيدَا إِصْلَاحًا يُوَفِّقِ اللَّـهُ بَيْنَهُمَا
“Mkikhofu mafarikiano baina yao, basi pelekeni hakimu kutoka watu wake mume na hakimu kutoka watu wake mke. Wakitaka suluhu, basi Allaah atawawafikisha kati yao.” (03:35)
Ikiwa kwa mfano hamhudumii vizuri, au mume ana tabia mbaya; ndugu wa mume walio karibu nae na ndugu wa mke walio karibu nae waangalie suala hili. Na ikiwa mke anamchukia mume, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia mwanamke mmoja:
“Je, umemrudishia (mume wako) haki yake? Akasema “Ndio”.
Akamuamrisha aachane nae.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1034
- Imechapishwa: 12/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
11. Sababu ya saba ya talaka ambayo ni kung´ang´ania mume ampe talaka
07 – Mke kumuomba na kumg´ang´ania mume amwache Anamuomba mume wake talaka wakati anapoingia na wakati anapotoka. Masikini huyu hajui kuwa ameingia katika dhambi kubwa asipokuwa na sababu inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametahadharisha jambo hilo na akawatishia Maswahabah zake. Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh)…
In "at-Twalaaq - asbaabuhu wa ´ilaajuh - Shaykh Jamal bin Furayhaan"

Mke kuomba talaka kwa mume wake bila ya sababu yoyote
https://www.youtube.com/watch?v=5GIHzJs8Bio Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuomba Talaka kwa mume wake na lini anaweza kuomba? Jibu: Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Mwanamke yeyoye atakayeomba Talaka kutoka kwa mume wake bila ya sababu yoyote, ni kaharamishiwa harufu ya Pepo." Tunachomnasihi ni yeye kuwa na subira, na subira…
In "Khul´ (Mwanamke kujivua katika ndoa)"
Mwanamke kama huyu ni haramu kwake harufu ya Pepo
Swali: Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema: “Mwanamke yeyote ambaye atamuomba mume wake talaka pasi na kosa basi ni haramu juu yake harufu ya Pepo.” Je, mwanaume akioa juu yake mwanamke wa pili ni miongoni mwa sababu au kosa la kumfanya yeye kuomba talaka kwa sababu…
In "Uoaji wa wake wengi"