Swali: Tunaomba ufafanuzi wa Hadiyth hii:

“Mwanamke yeyote ambaye atamuomba mume wake talaka bila ya sababu, basi ni haramu juu yake harufu ya Pepo.”

Jibu: Ufafanuzi ni kuwa, mwanamke asli yake ni mpungufu wa akili na dini. Kutokana na hili ndio Allaah akaifanya talaka kuwa kwenye mikono ya mwanaume. Vinginevyo, kila wakati mume anapomuudhi angemuomba mwanamke waachane. Lau Allaah angeiweka talaka kwenye mikono ya wanawake, basi mwanamke angelikuwa anamtaliki mume wake kwa siku mara ishirini. Allaahu ndiye mwenye kutakwa msaada. Mwanamke ni mpungufu wa akili na Dini kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akimuomba mume wake talaka na hakumfanyia jambo lolote baya, basi mwanamke huyo hatonusa harufu ya Pepo. Ama ikiwa mume anamfanyia mabaya, au mke akawa anamchukia na hawezi kumtekelezea haki zake, hapo anaweza kumuomba talaka. Ama ikiwa mume anamfanyia mabaya. Hakika Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُوا حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَا إِن يُرِيدَا إِصْلَاحًا يُوَفِّقِ اللَّـهُ بَيْنَهُمَا

“Mkikhofu mafarikiano baina yao, basi pelekeni hakimu kutoka watu wake mume na hakimu kutoka watu wake mke. Wakitaka suluhu, basi Allaah atawawafikisha kati yao.” (03:35)

Ikiwa kwa mfano hamhudumii vizuri, au mume ana tabia mbaya; ndugu wa mume walio karibu nae na ndugu wa mke walio karibu nae waangalie suala hili. Na ikiwa mke anamchukia mume, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia mwanamke mmoja:

“Je, umemrudishia (mume wako) haki yake? Akasema “Ndio”.

Akamuamrisha aachane nae.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1034
  • Imechapishwa: 12/08/2020