Salaf (Rahimahumu Allaah) walikuwa wakali kwa ajili tu ya kuacha baadhi ya mambo ya Sunnah au moja kwa moja wanamsema vibaya yule mwenye kuziacha. Kwa sababu kuna khatari akaguswa na kuenea kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuzipa mgongo Sunnah zangu basi si katika sisi.”[1]

Ndio maana Imaam Ahmad akasema:

“Anayeacha Witr huyo ni mtu muovu. Haitakikani kukubali ushahidi wake.”[2]

Kila kilichothibiti kutoka katika Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi tunajitahidi kwelikweli kukitendea kazi na kuwafunza nacho watu. Pengine kwa kufanya hivo Allaah akatupa thawabu za wale wenye kuzifufua Sunnah.

[1] al-Bukhaariy (5063) na Muslim (1401).

[2] ”ar-Rawdhw al-Murbiy´”, uk. 84 ya Buhuutiy.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 52
  • Imechapishwa: 12/08/2020