Kuna faida nyingi zisizodhibitika kwa ajili ya kutilia umuhimu Sunnah. Miongoni mwazo ni:

1- Yule mwenye kushikamana nazo anafikia ngazi ya kupendwa ambayo Allaah (´Azza wa Jall) amesema juu yake katika Hadiyth ya kiungu:

“Mja hatoacha kujikurubisha Kwangu kwa ´ibaadah za nawaafil mpaka mwishowe nije kumpenda. Nikimpenda basi huwa masikio yake yanayosikilizia, macho yake anayoonea, miguu yake anayotembelea nayo, mikono yake anayonyoshea, lau angeniomba kitu basi ningempa, lau angeniomba kinga basi ningelimkinga.”[1]

2- Miongoni mwa faida za kushikamana na Sunnah ni kwamba kunayaunga yale mambo ya faradhi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika jambo la kwanza watalofanyiwa hesabu watu kwalo siku ya Qiyaamah katika matendo yao ni swalah. Allaah (Ta´ala) atasema kuwaambia Malaika Wake: “Zitazameni swalah za mja wangu kama amezikamilisha au amezifanyia mapungufu? Ikiwa zimekamilika basi ataandikiwa nazo kamilifu. Na ikiwa kumepungua kitu, basi Atasema: “Mkamilishieni mja wangu faradhi Zake kutoka katika sunnah zake.”[2]

3- Yule mwenye kushikamana barabara na Sunnah katika zama za mwisho anao ujira mkubwa. ´Utbah bin Ghazwaan amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika huko mbele yenu kuna masiku ya subira; anayeshikamana kipindi hicho na kile mlichonacho nyinyi ana ujira wa watu khamsini katika nyinyi.” Akasema: “Ee Nabii wa Allaah! Au ni katika wao?” Akasema: “Bali katika nyinyi.”[3]

[1] al-Bukhaariy (6502).

[2] Abu Daawuud (864).

[3] Abu Daawuud (4341). Ameisahihisha al-Albaaniy katika ”Swahiyh wa Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud”.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 50-52
  • Imechapishwa: 12/08/2020