Swali: Je, nia ni kwa kutamka kwa mdomo wakati ninapotaka kutawadha au wakati ninapotaka kufunga Ramadhaan kila siku niseme: ”Nanuia kufanya jambo fulani” au inatosha kunuia ndani ya moyo? 

Jibu: Nia ni kile kitendo chako cha kufanya jambo. Wakati unapoamka usiku na kula daku kwa ajili ya kufunga, hiyo ndio nia yako. Unapoamka kwa ajili ya kuswali, hiyo ndio nia. Nia inakuwa moyoni pale anapotambua kuwa ameamka kwa ajili ya jambo hilo au ameanza kulifanya jambo hilo au atalifanya jambo hilo kwa ajili ya Allaah (Ta´ala). Hakuna haja ya kutamka kwa sauti kama kusema ´Nimenuia kwa ulimi wangu`. Bali atanuia kwa moyo wake na hivyo inatosha. Kuhusu kutamka kwa sauti kwamba amenuia kuswali na kwamba amenuia kutufu ni Bid´ah isiyokuwa na msingi. 

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/10736/حقيقة-النية-في-العبادات
  • Imechapishwa: 12/11/2023