Idadi ya chini kabisa ya kutekeleza swalah ya ijumaa

Swali: Nimesoma katika baadhi ya vitabu ya kwamba miongoni mwa sharti za kutekeleza swalah ya ijumaa ni kuwepo kwa watu arobaini katika wale ambao inawawajibikia swalah ya ijumaa. Gazeti la “ad-Da´wah” limesambaza fatwa yako muheshimiwa ya kwamba swalah ya ijumaa inatekelezwa kwa kuwepo watu wawili pamoja na imamu. Vipi kuoanisha kati ya fatwa hizo mbili? 

Jibu: Uwajibu wa kutekeleza swalah ya ijumaa kwa kuwepo watu arobaini ni maoni yaliyosemwa na kikosi cha wanazuoni akiwemo Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah). Lakini maoni yaliyo na nguvu zaidi ni kwamba inafaa kuitekeleza kwa idadi chini ya arobaini. Idadi ya chini kabisa ni watu watatu, kama ilivyotangulia katika fatwa wakati nilipojibu swali kabla ya hili. Hakuna dalili ya kushurutisha watu arobaini. Hadiyth inayosema kuwa watu arobaini ni sharti ni dhaifu. Hayo yamewekwa wazi na Haafidhw Ibn Hajar katika “Buluugh-ul-Maraam”. 

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mjmuu´-ul-Fataawaa (12/327)
  • Imechapishwa: 12/11/2023