Swali: Ikhwaaniy mmoja ameniuliza ni kwa nini tunajiita Ahl-us-Sunnah. Je, jina hilo limezushwa?

Jibu: Halikuzuliwa. Allaah anajua namna ambavo nilikuwa nikisita kutumia jina hilo kwa kuchelea kutolitendea kazi ipasavyo. Mpaka hii leo nachelea hivo. Imaam Ahmad bin Hanbal anazingatiwa kuwa ni imamu miongoni mwa maimamu wa Ahl-us-Sunnah. Kabla yake kuna Sufyaan ath-Tawriy, Maalik bin Anas na Ibn ´Abbaas. Jina hilo limtumiwa tokea wakati wa Ibn ´Abbaas. Muhammad bin Siyriyn amesema:

“Hawakuwa wakiuliza kuhusu cheni za wapokezi mpaka wakati kulipotokea fitina. Hapo ndipo tukawa tunasema: “Tutajieni wanaume wenu.” Wakawa wanatazamwa Ahl-us-Sunnah na kukachukuliwa kutoka kwao na wakitazamwa Ahl-ul-Bid´ah na hakuchukuliwi kutoka kwao.”

Kwa hiyo jina hilo ni la tangu zamani. Himdi zote njema zinamstahikia Allaah ni pigo dhidi ya al-Ikhwaan al-Muslimuun ambao wamejaribu kwa njia zote kusema kuwa jina hilo linawakimbiza watu mbali. Je, jina hilo linawakimbiza watu mbali au linawafanya watu kupenda ulingano huu? Baadhi ya maduka na wachapishaji vitabu Misri wanaitwa “as-Sunnah” na “as-Salafiyyah” kwa sababu ya kutaka kuwavutia watu ilihali wao wenyewe hawana lolote kuhusiana na jina hilo. Nyoyo za waislamu zimeumbwa katika maumbile ya kuzipenda Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunamuomba Allaah atuthibitishe na atufishe kutokana na Sunnah.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 71
  • Imechapishwa: 30/01/2025