Hapa ndipo itafaa kwa mswaliji kujitenga na imamu

Swali: Imamu akirefusha katika Maghrib na kwa mfano akasoma Aal ´Imraan. Baadaye akaja mtu na kujiunga na huku yuko na kazi. Je, anaweza kutoka nje ya swalah?

Jibu: Akiwa ni shuguli muhimu. Ni kama yule Swahabah ambaye aliswali nyuma ya Mu´aadh na wakati aliporefusha swalah akajitenga. Alikuwa na mazao na akachelea juu yake na baadaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akampa udhuru. Kwa hivyo ni sawa ikiwa ni urefu mkubwa unaowatia watu uzito.

Swali: Wakati mwingine imamu anarefusha ambapo watu wakakaa chini. Je, wakemewe?

Jibu: Wakiwa si wenye kuweza kusimama hapana vibaya. Ni sawa ikiwa kunawatia uzito. Wasikemewe. Kwa sababu katika watu wako ambao ni wazee na wengine wanyonge. Ambaye yuko na nguvu asiketi chini. Haijuzu kwake kukaa chini katika swalah ya faradhi. Asiketi chini. Lakini ni sawa ikiwa ni kisimamo cha Ramadhaan kama vile Tahajjud.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22636/هل-يجوز-الخروج-او-الجلوس-لو-اطال-الامام
  • Imechapishwa: 11/07/2023