72 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia, kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hazini mwenye kuzini hali ya kuwa ni muumini, na wala haibi pale anapoiba hali ya kuwa ni muumini.”[1]

73 –  Abu Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Tha´labah, kutoka kwa Abu Qilaabah: mjumbe, aliyemuuliza ´Abdullaah bin Mas´uud, amenihadithia:

“Nakuuliza kwa jina la Allaah: Unajua kama kipindi cha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) watu walikuwa wamegawanyika mafungu matatu: muumini wa siri, muumini waziwazi na kafiri wa siri na kafiri wa waziwazi?” ´Abdullaah akasema: “Ndio, naapa kwa Allaah!” Nakuuliza kwa jina la Allaah: Wewe ulikuwa katika wepi?” Akasema: “Nilikuwa muumini wa siri na muumini wa waziwazi – mimi ni muumini.” Abu Ishaaq[2] amesema: “Nikakutana na ´Abdullaah bin Mughaffal na kusema; “Kuna watu wema wanaonikemea mimi kusema kuwa ni muumini.” Ndipo ´Abdullaah bin Mughaffal akasema: “Umeangamia na kukhasirika usipokuwa muumini.”

74 – Abu Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa Muusa bin Muslim ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Ibraahiym at-Taymiy[3] ambaye amesema:

“Kuna tatizo gani mtu akisema kuwa ni muumini? Naapa kwa Allaah! Akiwa ni mkweli basi Allaah hatomuadhibu juu ya ukweli wake, na akiwa ni mwongo, basi ukafiri aliyoingia ni mbaya zaidi kuliko uwongo.”

75 – Abu Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Ibraahiym ambaye amesema:

“´Alqamah aliulizwa kama ni muumini. Akajibu: “Nataraji hivo.”

[1] Cheni ya wapokezi ni kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Hadiyth kama hiyo imekwishatangulia (38) kutoka kwa Abu Hurayrah.

[2] Bi maana ash-Shaybaaniy aliyetajwa katika cheni ya wapokezi. Jina lake ni Sulaymaan bin Abiy Sulaymaan al-Kuufiy. Alikuwa ni mwaminifu na hoja. Usimuliaji wake wa cheni ya wapokezi kwenda mpaka kwa Ibn Mughaffal ambaye ni Swahabah anayetambulika ni Swahiyh. Lakini ni dhaifu kwenda mpaka kwa Ibn Mas´uud, kwa sababu mjumbe hajulikani. Kinachodhihiri ni kwamba Tha´labah ni Ibn Yaziyd al-Himmaaniy al-Kuufiy, ambaye alikuwa mkweli na sifa za Tashayyu´. Yahyaa bin Sa´iyd ameipinga Athar hii kutoka kwa Ibn Mas´uud, kama alivotaja Abu ´Ubayd (42) katika “Kitaab-ul-Iymaan”.

[3] Ibraahiym bin Yaziyd bin Shariyk at-Taymiy; alikuwa mwanafunzi wa Maswahabah, mwaminifu na mfanya ´ibaadah. Cheni ya wapokezi kwake ni Swahiyh. Muusa bin Muslim ash-Shaybaaniy alikuwa akitambulika kama Muusa as-Swaghiyr.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 11/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy