Swali: Anayeshikamana na Sunnah barabara kama inavyotakikana kwa njia ya kwamba akafupisha nguo yake na akafuga ndevu zake, basi waislamu wengi wanasema kuwa ana msimamo mkali na mwenye kuchupa mipaka. Mtu ashike msimamo gani?

Jibu: Awapuuze. Awaeleze kuwa ni Sunnah na kuwaombea kwa Allaah awaongoze. Awazungumzishe kwa maneno mazuri. Awaombee kwa Allaah awaongoze na kuwaeleza kuwa ni Sunnah. Awafunze kwa dalili. Hawatomdhuru na asiwajali. Ni kama walivofanya wanafiki kwa watu wa Sunnah:

وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ

”Na wanapowapitia [karibu yao], basi wanakonyezana.”[1]

[1] 83:30

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22640/كيف-يعامل-من-يصف-السنة-بالتشدد-والتزمت
  • Imechapishwa: 11/07/2023