Hapa ndipo inaruhusiwa kwa mwanamke kufunga kizazi

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kufanya upasuaji wa kuondosha kizazi ikiwa anadhurika kwa kushika mimba?

Jibu: Ikiwa kuna madhara ya wazi, basi awashauri madaktari bingwa wa kiume na madaktari bingwa wa kike. Ikiwa kuna madhara ya wazi hapana vibaya kuondosha kizazi.

Muulizaji: Anataka kuondosha kizazi?

Ibn Baaz: Ni lazima kuwepo na uhakika wa madhara na isiwe mahisio tu.

Swali: Kukiwepo na uhakika aondoshe kizazi?

Jibu: Hapana vibaya. Aondoshe au afunge.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23272/هل-يجوز-تعقيم-المراة-المتضررة-بالحمل
  • Imechapishwa: 15/12/2023