Swali: Je, inafaa kutibu uchawi kwa kutumia uchawi?

Jibu: Hapana. [´Imraan bin Huswayn (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:]

”Si katika sisi yule atakayeamini mikosi au akaomba kubashiriwa mikosi, akafanya uchawi au akafanyiwa uchawi, akafanya ukuhani au akafanyiwa ukuhani.”[1]

Kutibu uchawi kwa uchawi ni haramu. Hakuna anayefumbua uchawi isipokuwa mchawi. Haijuzu kufanya hivo. Uchawi unatibiwa kwa njia zinazoruhusiwa, kama vile dhikr, Qur-aan na du´aa zinazotambuliwa na wale wenye taaluma hiyo.

[1] al-Bazzaar (3578), ad-Duulaabiy (2083) na at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw” (355).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 15/12/2023