Hapa jihaad inakuwa faradhi kwa watu wote

Swali: Je, jihaad inaweza kuwa faradhi kwa watu wote kama mfano wa swawm kama alivosema Allaah (Ta´ala):

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ

“Na haiwapasi waumini watoke wote pamoja kwenda [kupigana vita vya jihaad]. Basi kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao, kundi [moja] wajifunze dini na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kutahadhari.”[1]?

Jibu: Ni faradhi kwa baadhi ya watu.

Swali: Je, jihaad inaweza kuwa faradhi kwa watu wote kama vile swalah na swawm?

Jibu: Wanazuoni wamesema pindi mtu anapokuwa kati ya safu mbili, akateuliwa na kiongozi au wakavamiwa na adui, katika hali hizo jihaad inakuwa faradhi kwa watu wote.

[1] 09:122

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22880/متى-يكون-الجهاد-فرض-عين-او-فرض-كفاية
  • Imechapishwa: 09/09/2023