Swali: ´Ibaadah za kimwili kama vile swalah ndio bora au jihaad?

Jibu: Jihaad ni bora. ´Ibaadah bora inayopendeza ni jihaad. Jihaad inaiweka nafsi na mali khatarini. Elimu pia ni katika jihaad. Kujifunza elimu sio ´ibaadah inayopendeza tu, ni lazima. Kujifunza elimu ni wajibu.

Swali: Elimu inayotosheleza?

Jibu: Kujifunza elimu inayomfanya mtu kuitambua dini yake na yale ambayo Allaah amemuwajibishia na kumuharamishia ni wajibu. Kuhusu elimu yenye kuzidi hapo jihaad ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22875/هل-الجهاد-افضل-من-ساىر-العبادات-البدنية
  • Imechapishwa: 09/09/2023