Swali: Ni vipi hali ya wale watenda madhambi ambao wataingizwa Motoni na baadaye kutolewa humo?

Jibu: Wako mafungu mbalimbali na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Wako ambao wanaadhibiwa na wasioadhibiwa, wengine wanaadhibiwa baadhi ya nyakati na kuachwa. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amewaweka katika maisha ya ndani ya kaburi yanayoitwa ”Dhuu Shaa-ibatayn”. Kumetajwa hali za waumini na kusalimika kwao na hali za makafiri na kuadhibiwa kwao.

Kuhusu ”Dhuu Shaa-ibatayn” – ambao ni wale watenda madhambi – maandiko mengi yamewanyamazia katika hali ya ndani ya kaburi. Baadhi ya maandiko yamebainisha yatayowapata ndani ya kaburi kama vile yule anayeadhibiwa ndani ya kaburi kwa sababu ya kutojichunga kutokana na cheche za mkojo na yule ambaye anaadhibiwa kwa sababu ya umbea.

Kwa kifupi ni kwamba wako katika khatari ya kuadhibiwa ndani ya Moto na ndani ya kaburi kote kuwili. Hata hivyo wao sio makafiri ambao adhabu yao ni ya hakika. Kuhusu watenda madhambi pengine baadhi yao wakasamehewa kutokana na matendo yao mema ambayo yameshinda uzito matendo yao maovu. Huenda vilevile wakaadhibiwa baadhi ya nyakati kisha wakasamehewa, pengine adhabu yao ikacheleweshwa hadi wakati wa Motoni. Allaah (Jalla wa ´Alaa) ndiye mwenye kuamua cha kuwafanya. Upambanuzi wa jambo lao ni kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24378/هل-تتفاوت-احوال-العصاة-في-القبور
  • Imechapishwa: 06/10/2024