Swali: Wako wanaosema kuwa wale watu 70.000[1] ndio bora zaidi?
Jibu: Ubora huu ambao Allaah kawafanya kuwa maalum kwao haupelekei kwamba wao ni bora kuliko wale wanaowashinda. Hata hivyo ndani yake kuna fadhilah ya kwamba wataingia Peponi pasi na hesabu. Isitoshe jambo hilo linatofautiana. Wote wakiwa mamilioni wanaweza kuingia Peponi bila ya hesabu, lakini daraja za baadhi zikawa juu zaidi kuliko za wengine. Kwa mfano as-Swiddiyq ataingia Peponi bila ya hesabu na vivyo hivyo ´Umar ataingia pasi na hesabu. Licha ya kwamba as-Swiddiyq ni bora kuliko ´Umar. Kitendo cha wao kuingia Peponi bila ya hesabu haina maana kwamba hali yao ni moja. Ni jambo linalotambulika kwamba wale 70.000 na mamilioni ya watu wakaingia Peponi bila ya hesabu. Hata hivyo ubora wao na nafasi zao mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) zikatofautiana.
[1] Tazama https://firqatunnajia.com/3-mwenye-kuhakikisha-tawhiyd-basi-ataingia-peponi-bila-ya-hesabu/
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24374/هل-السبعين-الفا-افضل-ممن-سواهم
- Imechapishwa: 06/10/2024
Swali: Wako wanaosema kuwa wale watu 70.000[1] ndio bora zaidi?
Jibu: Ubora huu ambao Allaah kawafanya kuwa maalum kwao haupelekei kwamba wao ni bora kuliko wale wanaowashinda. Hata hivyo ndani yake kuna fadhilah ya kwamba wataingia Peponi pasi na hesabu. Isitoshe jambo hilo linatofautiana. Wote wakiwa mamilioni wanaweza kuingia Peponi bila ya hesabu, lakini daraja za baadhi zikawa juu zaidi kuliko za wengine. Kwa mfano as-Swiddiyq ataingia Peponi bila ya hesabu na vivyo hivyo ´Umar ataingia pasi na hesabu. Licha ya kwamba as-Swiddiyq ni bora kuliko ´Umar. Kitendo cha wao kuingia Peponi bila ya hesabu haina maana kwamba hali yao ni moja. Ni jambo linalotambulika kwamba wale 70.000 na mamilioni ya watu wakaingia Peponi bila ya hesabu. Hata hivyo ubora wao na nafasi zao mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) zikatofautiana.
[1] Tazama https://firqatunnajia.com/3-mwenye-kuhakikisha-tawhiyd-basi-ataingia-peponi-bila-ya-hesabu/
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24374/هل-السبعين-الفا-افضل-ممن-سواهم
Imechapishwa: 06/10/2024
https://firqatunnajia.com/wale-70-000-ni-bora-kuliko-wengine/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)