Hakupelekei kheri wala shari yoyote

Swali: Je, mtenda madhambi anaweza kumuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Je, kuna fadhilah katika kumuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayeniona basi ameniona kweli. Kwani hakika shaytwaan hawezi kujifananisha na mimi.”

Swali: Baadhi yao wanasema kuwa wamemuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Katika jambo la kumuona hakupelekei katika kheri wala shari yoyote. Wako wengi waliomuona katika maisha yake na wakafa katika ukafiri. Kwa msemo mwingine hakukuwafaa kitu kule kumuona kwao. Wanafiki hakukuwafaa kitu kumuona. Wale walioritadi baada ya kufa kwake hakukuwafaa kitu kumuona.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23377/%D9%87%D9%84-%D9%8A%D8%B1%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D8%A7%D8%B5%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A-%EF%B7%BA-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%86%D8%A7%D9%85
  • Imechapishwa: 05/01/2024