Hakuna haja ya wanajimu na wataalamu wa wakati

Copts wamebobea katika hesabu, algebra na mambo mengine yanayopoteza muda. Wanajimu wamebobea juu ya kutembea kwa nyota, mwezi, jua, kupatwa kwa jua na miunganiko ya jua. Ubobeaji ambao haukuwekwa na Shari´ah. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotaja miezi na utambuzi wa miandamo yake, alibainisha kuwa utambuzi wake si kwa njia wanayotumia wanajimu na wataalamu wa wakati na kwamba jambo hilo hatulijali katika dini yetu na kwamba kamwe hatuhesabu mwezi kwa njia hiyo. Kisha akabainisha kuwa mwezi unathibiti kwa njia ya kuoenekana peke yake ambapo ima unaingia kwa siku ishirini na tisa au kwa kukamilisha siku thelathini. Kwa kutimiliza siku thelathini hatuhitajii kujikakama kuuona mwezi mwandamo.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/191-192)
  • Imechapishwa: 10/11/2020