Jambo la wajibu kwa madaktari wanaowatibu wanawake

Swali: Mimi nina kazi ambayo ni kudunga sindano za matibabu ambapo najiliwa na wagonjwa wa kiume na wa kike. Wakati wa kudunga sindano hizo mimi hugusa miili ya wanawake. Je, katika hili kuna kitu katika haramu?

Jibu: Hakuna kitu katika haramu haja ikipelekea kufanya hivo ikiwa maeneo hayo hakuna zaidi ya mwanaume huyu anayedunga sindano. Akiwepo mwanamke ambaye anaweza kufanya kazi hiyo basi haitojuzu kwa mwanamme kufanya hivo. Isitoshe ikifaa kufanya hivo wakati wa haja basi ni lazima kwake asiwe na hisia za matamanio au ngozi kutetemeka wakati wa kugusa mwili wa mwanamke. Bali ajihisi mwenyewe kuwa ni daktari mwenye kutibu ili aepuke sehemu ya fitina.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (07) http://binothaimeen.net/content/6712
  • Imechapishwa: 10/11/2020