28. Twubaa kwa Ghurabaa wanaowatengeneza watu na wanayoharibu

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ibn Wadhdhwaah amepokea maana kama hiyo kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa muundo:

“Baada yenu kunakuja masiku ambayo yule aliyeshikamana na yale mnayofanya nyinyi hii leo analipwa ujira wa wanaume khamsini katika nyinyi.”

Kisha akasema: “Muhammad bin Sa´iyd ametueleza: Asad ametueleza: Sufyaan bin ´Uyaynah ametukhabarisha, kutoka kwa Aslam al-Baswriy, kutoka kwa Sa´iyd, nduguye al-Hasan, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nilisema kumwambia Sufyaan: ”Haya yanatoka kwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?” Akasema: “Ndio.” Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hii leo mko katika ushahidi wa wazi kutoka kwa Mola Wenu, mnaamrisha mema, mnakataza maovu na mnapigana Jihaad katika njia ya Allaah na hamjasibiwa na vilevi viwili ambacho ni kilevi cha ujinga na kilevi cha kupenda maisha. Hata hivyo mtakuja kubadilika muache kuamrisha mema, kukataza maovu, kupigana Jihaad kwa ajili ya Allaah na mtasibiwa na vilevi viwili. Siku hiyo yule mwenye kushikamana barabara na Kitabu na Sunnah analipwa ujira khamsini.” Wakasema: “Katika sisi?” Akasema: “Hapana. Katika nyinyi.”[1]

Amepokea kwa mlolongo wa wapokezi kupitia kwa al-Mu´aafiriy ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Twubaa kwa wageni wenye kushikamana na Kitabu pindi kinapoachwa na wanaitendea kazi Sunnah pindi inapozimwa!”[2]

MAELEZO

Hwa ndio wageni ambao wanatengeneza pindi watu wameharibika na pia wanatengeneza yale yaliyoharibiwa na watu kwa kuamrisha mema na kukataza maovu na wanashikamana barabara na Qur-aan pindi itakapoachwa na watu:

“Uislamu ulianza ni kitu kigeni na utarudi kuwa kitu kigeni kama ulivyoanza. Hivyo Twubaa kwa wale wageni!”

Wageni ndio watu wenye kutengeneza na wenye msimamo ambao wanatekeleza maamrisho na wanalingania katika dini ya Allaah wakati wa kuharibika kwa wakati na kubadilika watu.

[1] al-Bid´ah, uk. 133.

[2] al-Bid´ah, uk. 122.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 50-51
  • Imechapishwa: 10/11/2020