709- Nilimsikia Ahmad akiulizwa juu ya mtu ambaye mtaji wake ni vipande vya dhahabu 20 na pia yuko na familia; je, analazimika kuhiji?” Akajibu:

“Nataraji kwamba hajj haimlazimu. Akihiji basi familia yake inaangamia.”

Bi maana kutokea Baghdaad.

710- Ahmad aliulizwa kuhusu mwanamme ambaye yuko na pesa za kuoa; je, aoe au ahiji kwa pesa hizo? Akajibu:

“Ahiji kama hachelei kufanya dhambi.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 150
  • Imechapishwa: 26/03/2021