728- Ahmad ametuhadithia: Raawh ametuhadithia: Sa´iyd ametuhadithia, kutoka kwa Qataadah ambaye hakuonelea vibaya mwanamke kuvaa pete au mahereni wakati anapokuwa katika Ihraam. Hata hivyo alichukizwa na kuvaa vikuku, vicheni vya mikono na vicheni vya miguuni.

729- Ahmad ametuhadithia: Hushaym ametuhadithia, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym aliyechukizwa na mwanamke kuvaa mapambo yenye kuonekana wakati wa Ihraam.

730- Ahmad ametuhadithia: Yahyaa Ahmad ametuhadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah, kutoka kwa Naafiy´ ambaye amesema:

“Wanawake na wasichana wa ´Abdullaah walikuwa wamevaa mapambo na mavazi yaliyotiwa zafarani wakati walipokuwa katika Ihraam. ´Abdullaah hakuwakemea jambo hilo.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 154
  • Imechapishwa: 26/03/2021