738- Ahmad ametuhadithia: Hushaym ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Malik na al-Hajjaaj, kutoka kwa ´Atwaa´ ambaye amesema:

“Yule ambaye atafunika kichwa chake kwa kusahau hakuna kinachomlazimu. Na yule mwenye kufanya hivo kwa kukusudia anatakiwa kutoa kafara.”

739- Ahmad ametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Jurayj, kutoka kwa ´Atwaa´ ambaye amesema:

“Kusahau na ujinga ni kitu kimoja. Hakuna kinachomlazimu mwenye kuvaa mavazi au kujitia manukato.”

Bi maana yule mwenye kufanya hivo kwa kusahau.

741- Ahmad ametuhadithia: Hushaym ametuhadithia, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym ambaye amesema:

“Muhrim akiamka na kichwa chake kimefunikwa, basi anatakiwa kukifunua. Hata hivyo hakuna kinachomlazimu kufanya. Anatakiwa kujishughulisha kufanya Talbiyah.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 156-157
  • Imechapishwa: 26/03/2021