Haikuthibiti kunyanyua mikono katika du´aa ya adhaana

Swali: Je, mtu anyanyue mikono juu wakati wa kuomba du´aa:

اللهم رب هذه الدعوة التامة والصلاة القائمة، آت محمداً الوسيلة والفضيلة، وابعثه مقاماً محموداً الذي وعدته

“Ee Allaah, Mola wa mwito huu uliotimia, swalah iliosimama, mpe bwana wetu Muhammad, al-Wasiylah na fadhilah na mfikishe daraja yenye kusifiwa ambayo umemuuahidi” basi utamthubutukia uombezi wangu siku ya Qiyaamah.”?

Jibu: Haikupokelewa. Sijui kama kumepokelewa kitu juu ya hilo.

Swali: Je, mtu anaweza kusema bora ni kuacha kufanya hivo?

Jibu: Ndio kinachodhihiri. Hakukupokelewa kuhusu du´aa hii kunyanyua mikono.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23695/حكم-رفع-اليدين-في-اللهم-رب-هذه-الدعوة
  • Imechapishwa: 05/04/2024