Shaytwaan wakati kunaposomwa Qur-aan na kuadhiniwa

Swali: Ni kwa nini shaytwaan hukimbia kunapoadhiniwa na hakimbii wakati kunaposomwa Qur-aan?

Jibu: Imetajwa katika Hadiyth ya kwamba hukimbia kunaposomwa Qur-aan pia:

“Hakika shaytwaan huikimbia nyumba ambayo kunasomwa ndani yake Suurah “al-Baqarah”.”

Swali: Je, hurudia baada ya adhaana kusikiliza swalah pamoja na wenye kuswali?

Jibu: Kwa ajili ya kuwashawishi – Allaah amlaani!

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23693/هل-يفر-الشيطان-من-القران-مثل-الاذان
  • Imechapishwa: 05/04/2024