Haikuhifadhiwa kwamba alipangusa uso wake

Swali: Vipi kufuta uso baada ya kumaliza kuomba du´aa?

Jibu: Kumepokelewa Hadiyth nyingi. Haafidhw (Rahimahu Allaah) amesema kuwa Hadiyth zote kwa mkusanyiko wake ni nzuri. Kwa hivyo ni sawa akipangusa. Hata hivyo bora ni mara kwa mara. Kwa sababu haikuhifadhiwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa upande wa kitendo chake. Hata hivyo ameelekeza juu ya hilo katika baadhi ya Hadiyth ambazo zinapeana nguvu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23128/هل-صح-المسح-على-الوجه-بعد-الدعاء
  • Imechapishwa: 09/11/2023