Swali: Muumini wa kike akimuona mmoja katika jamaa zake anafanya baadhi ya maovu amkemee vipi? 

Jibu: Ni lazima kwake akemee maovu kwa njia nzuri, maneno mazuri, upole na ulaini kwa yule anayemkemea. Kuna uwezekano akawa ni mjinga. Pengine akawa na maadili mabaya. Kila ambavyo anamkemea maovu kwa ukali ndivo yanazidi maovu yake. Kwa hiyo ni lazima kwake kukemea maovu kwa njia nzuri, maneno mazuri, dalili ya wazi kuhusu aliyosema Allaah na Mtume Wake sambamba na kumuombea kwa Allaah amuwafikishe. Lengo ni ili asimkimbize. Hivo ndivo inakuwa kuamrisha mema na kukemea maovu muda wa kuwa yuko na elimu, utambuzi, upole na ustahamilivu, mambo yanayomfanya yule anayekemewa maovu kukubali na hivyo asikimbie wala kufanya kiburi. Kwa hivyo ajitahidi aamrishe mema na kukataza maovu kwa kutumia matamshi ambayo kuna matarajio nyuma yake mlinganiwa kukubali haki. 

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/226)
  • Imechapishwa: 08/11/2023