Haijuzu kuwaendea wasomaji wenye kutumia jini

Swali: Napenda kukujuza ya kwamba Zambia kuna mtu muislamu anayedai kuwa ana jini. Watu wanamjia na wanamuomba dawa kwa maradhi yao mbalimbali. Huyu jini ndiye ambaye anawapangia dawa. Je, kitendo hichi kinajuzu? Mimi nimewaambia watu kuwa haijuzu pamoja na kuwa wananighadhibikia. Ninataraji kutumiwa fatwa haraka iwezekanavyo.

Jibu: Haijuzu kwa mtu huyo kutumia jini kama ambavyo haijuzu vilevile kwa watu kumwendea kumuomba awatibu maradhi yao kutokana na njia ya jini anayoitumia. Vilevile haijuzu kumwendea atatue mambo kwa njia kama hiyo. Matibabu kupitia njia ya matabibu ya wanaadamu kwa kutumia madawa yanayoruhusiwa ni jambo la sawa na lenye kutosheleza na kitendo hicho. Ukiongezea juu ya hilo ni kujisalimisha na ukuhani wa makuhani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwende kumwendea mpiga ramli akamuuliza juu ya kitu, basi swalah zake hazitokubalika kwa siku arubaini.”

Ameipokea Muslim katika kitabu chake “as-Swahiyh” yake.

Ahl-us-Sunan wane pamoja na al-Haakim ambaye ameisahihisha ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kumwendea kuhani na akamuuliza kwa aliyoyasema amekufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad.”

Mtu huyu na marafiki zake wa kijini wanazingatiwa ni katika wapiga ramli na makuhani. Hivyo haijuzu kuwauliza wala kuwasadikisha.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/409)
  • Imechapishwa: 24/08/2020