Hadiyth zote kuhusu fadhilah za I´tikaaf ni dhaifu

Swali: Ambaye atafanya I´tikaaf siku moja kwa ajili ya Allaah basi Allaah atafanyia baina yake na Moto mahandaki matatu?

Jibu: Hadiyth hii ni dhaifu. Hadiyth kuhusu fadhilah za I´tikaaf zote ni dhaifu. Kilichothibiti ni kwamba inapendeza. Kitendo cha yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alifanya I´tikaaf ndio kilichothibiti. Vilevile maneno Yake (Jalla wa ´Alaaa):

وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ

“Na wala msichanganyike nao hali ya kuwa nyinyi ni wenye kukaa I’tikaaf  misikitini.”[1]

Huu ndio msingi. Ama Hadiyth kuhusu fadhilah za I´tikaaf hatujui ambayo ni Swahiyh.

[1] 02:187

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22840/هل-صحت-احاديث-في-فضل-الاعتكاف
  • Imechapishwa: 08/09/2023