11. Hadiyth “Wakati mja atakaposafisha meno yake kwa Siwaak… “

215 – ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) alihimiza Siwaak na akaeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إن العبدَ إذا تَسَوَّك ثم قامَ يُصلي، قام الملَكُ خَلفه، فَيَستَمعُ لقراءتِه، فيدنو منه -أو كلمة نحوها- حتى يضعَ فاه على فِيه، فما يخرجُ من فيه شيءٌ من القرآنِ إلا صارَ في جوفِ الملَكِ، فَطَهَّروُا أفواهكم للقرآن

“Wakati mja atakaposafisha meno yake kwa Siwaak kisha akasimama kuswali, basi Malaika husimama nyuma yake na akasikiliza kisomo chake na akamkurubia mpaka akauweka mdomo wake juu ya mdomo wake. Hakuna chochote katika Qur-aan kinachotoka mdomoni mwake isipokuwa kinaingia ndani ya Malaika. Hivyo basi, hakikisheni mnaisafisha midomo yenu kwa ajili ya Qur-aan.”[1]

Ameipokea al-Bazzaar kwa cheni ya wapokezi nzuri. Ibn Maajah pia ameipokea sehemu yake kama maneno ya Swahabah, na pengine ndio sahihi zaidi[2].

[1] Nzuri na Swahiyh.

[2] Sivyo. Katika cheni ya wapokezi kwa Ibn Maajah kuna mkatiko na mpokezi mwenye kuachwa. Tazama ”as-Swahiyhah” (1213).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/204)
  • Imechapishwa: 15/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy