Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن ابن مسعود رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (إنَّ الصِّدقَ يَهْدِي إِلَى البرِّ، وإنَّ البِرَّ يَهدِي إِلَى الجَنَّةِ، وإنَّ الرَّجُلَ لَيَصدُقُ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ صِدِّيقًا. وَإِنَّ الكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الفُجُورِ، وَإِنَّ الفُجُورَ يَهدِي إِلَى النَّارِ، وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَكْذِبُ حَتَّى يُكتَبَ عِنْدَ الله كَذَّابًا). مُتَّفَقٌ عَلَيه

54 – Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika ukweli unaongoza katika wema na hakika wema unaongoza katika Peo na mtu ataendelea kusema ukweli mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni mkweli. Hakika uongo unaongoza katika uovu na uovu unaongoza katika Moto. Hakika mtu ataendelea kusema uongo mpaka aandikwe mbele ya Allaah kuwa ni mwongo.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Uongo ni haramu. Bali baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa ni katika madhambi makubwa kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametishia kuwa mtu anaandikwa mbele ya Allaah kuwa ni muongo.

Katika uongo mkubwa ni pamoja na yale yanayofanywa na baadhi ya watu  leo pale ambapo wanaleta khabari za uongo kwa ajili ya kutaka kuwachekesha watu. Kumekuja Hadiyth ya matishio juu ya hili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ole wake yule anayesema uongo ili awachekeshe watu. Ole wake! Ole wake!”[1]

Haya ni matishio kwa jambo ambalo watu wengi wamelichukulia kuwa ni jepesi.

Uongo wote na ni haramu. Uongo wote unapelekea katika uovu. Hakuvuliwi ndani yake kitu isipokuwa katika hali tatu, kama ilivyokuja katika Hadiyth; vitani, kupatanisha kati ya watu na wanandoa.

[1] Abu Daawuud (4990) na amesema kuwa ni Hasan

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/296-297)
  • Imechapishwa: 27/04/2023