Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أبي محمد الحسن بنِ عليِّ بن أبي طالب رضي الله عنهما قَالَ: حَفظْتُ مِنْ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ مَا يَرِيبُكَ إِلَى مَا لا يَرِيبُكَ؛ فإنَّ الصِّدقَ طُمَأنِينَةٌ، وَالكَذِبَ رِيبَةٌ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث صحيح))

55 – Abu Muhammad al-Hasan bin ´Abiy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema: “Nilihifadhhi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Acha linalotia shaka na ufanye lisilokutia shaka, ukweli ni utulivu na uongo ni shaka.” at-Tirmidhiy na amesema kuwa ni Swahiyh.

Ukweli ni utulivu. Kwa sababu mwenye kusema ukweli katu hajuti na kusema “laiti”. Ukweli ni uokovu. Wakweli Allaah huwaokoa kwa ukweli wao. Utamuona mtu mkweli daima anakuwa katika utulivu. Kwa sababu hajuti kwa kitu chenye kutokea au kitachotokea huko mbeleni kwa sababu amesema ukweli. Mwenye kusema ukweli ameokoka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/300)
  • Imechapishwa: 27/04/2023