Shahidi inapotoka roho yake hahisi maumivu

Shahidi anapouawa katika njia ya Allaah hahisi kipigo. Ni kana kwamba hakukupitika kitu. Anachohisi tu ni roho yake kutoka na kwenda katika neema zenye kudumu na za milele. Ndio maana amesema (Swala Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… na tambueni kuwa Pepo iko chini ya vivuli vya panga.”

Miongoni mwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) kuna anayeitwa Anas bin an-Nadhwar (Radhiya Allaahu ´anh) alisema:

“Mimi nahisi harufu ya Pepo chini ya [mlima wa] Uhud.”[1]

Tazama jinsi Allaah alivomuwezesha mpaka akaweza kunusa harufu ya kihakika ya Pepo. Baada ya hapo akapigana mpaka akauawa (Radhiya Allaahu ´anh).

[1]al-Bukhaariy (4047)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/285)
  • Imechapishwa: 27/04/2023