Hadiyth “Hakika mambo yalivyo subira wakati wake ni pale mwanzoni mwa kupatwa na msiba”

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: مَرَّ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بامرأةٍ تَبكي عِنْدَ قَبْرٍ، فَقَالَ: (اتّقِي الله واصْبِري) فَقَالَتْ: إِليْكَ عَنِّي؛ فإِنَّكَ لم تُصَبْ بمُصِيبَتي وَلَمْ تَعرِفْهُ، فَقيلَ لَهَا: إنَّه النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَتَتْ بَابَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فَلَمْ تَجِدْ عِنْدَهُ بَوَّابينَ، فقالتْ: لَمْ أعْرِفكَ، فَقَالَ: (إنَّمَا الصَّبْرُ عِنْدَ الصَّدْمَةِ الأُولى). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

وفي رواية لمسلم: (تبكي عَلَى صَبيٍّ لَهَا).

31 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpitia mwanamke ambaye alikuwa analia kwenye kaburi na kumwambia: “Mche Allaah na kuwa na subira!” Akasema: “Niondokee, hujafikwa na msiba ulonifika!” [na mwanamke huyo] hakumtambua [aliyemwambia vile].  Akaambiwa: “Huyo alikuwa ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akaenda mpaka kwenye mlango wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hakukua walinzi. Akamwambia: “Sikukutambua.” Akasema: “Hakika mambo yalivyo subira wakati wake ni pale mwanzoni mwa kupatwa na msiba.”[1]

Mtu akisema mwanamke kutembelea makaburi si ni jambo limeharamishwa? Ndio. Ni haramu kwa wanawake. Bali ni katika madhambi makubwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kutembelea makaburi na wale wenye kuyafanya ni mahala pa kuswali na kuyawekea mataa[2]. Lakini hata hivyo mwanamke huyu hakutoka kwenye kutembelea makaburi. Alitoka kutokana na uchungu na huzuni mkubwa aliyokuwa nao moyoni mwake kwa kufariki kwa mtoto huyu. Hakuweza kuimiliki nafsi yake kutokutoka. Kwa ajili hii ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akampa udhuru na hakukabiliana naye kwa nguvu wala kumlazimisha arudi nyumbani kwake.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

[2]at-Tirmidhiy (320), an-Nasaa´iy (2043)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/227-228)
  • Imechapishwa: 21/02/2023