Uhakika wa mambo ni kwamba tanzia sio kupeana hongerakama wanavofikiria watu wa kawaida. Hivyo wanasherehekea hilo kwa kufanya na kuandaa mambo mbalimbali. Hili ni kosa. Kutoa rambirambi ni kumtuliza aliyefikwa na msiba awe na subira. Kwa ajili hii lau mtu hakufikwa na msiba, kwa mfano mtu amefiwa na mtoto wa ami yake na hilo halikumtikisa, hapewi mkono wa pole. Kwa ajili hii ndio maana wanazuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema:

“Imenusiwa kumpa mkono wa pole yule aliyefikwa na msiba.”

Hawakusema kuwa imesuniwa kumpa pole ndugu. Kwa sababu huenda ndugu asitikiswe kwa kufa ndugu yake na badala yake hilo likamtikisa mtu wa mbali [asiyekuwa ndugu]. Hilo ni kutokana kwa mfano na uhusiano imara waliokuwa nao.

Kwa hivyo tanzia anapewa yule mwenye kutikiswa na msiba na si ndugu. Lakini leo mambo yamegeuka. Pole imekuwa anapewa tu ndugu. Anapewa pole hata kama hilo litakuwa limemfanya kufurahi kwa kufa yule ndugu yake. Huenda mtu akawa ni fakiri na baina yake yeye na mtoto wa ami yake kuna mizozo. Binamu yake akafa na ameacha mamilioni ya pesa. Je, katika hali hii atasikitika kwa kufa kwa binamu yake au atafurahi? Asilimia kubwa ni kwamba atafurahi na kusema namshukuru Allaah kwa kunitoa kwenye matatizo na kunirithisha mali zake. Huyu hapewi pole. Huyu lau tutataka kumwambia kitu basi tutampa hongera.

Lililo muhimu ni wajibu kujua ya kwamba rambirambi imewekwa kwa ajili ya kumtia nguvu aliyefikwa na msiba ili awe na subira na kumliwaza. Mtu achague maneno yaliyo bora kabisa iwezekanavyo ambayo yanasemwa wakati wa kutoa pole. Hakuna maneno yaliyo bora zaidi kuliko yale aliyoweka Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/209-210)
  • Imechapishwa: 21/02/2023