Fuata dalili na usifuate matamanio yako!

Swali: Ikiwa wanachuoni wametofautiana juu ya maovu fulani, kuko waliohalalisha na wengine wameharamisha. Je, ni wajibu…

Jibu: Wewe usitazame maoni mbali mbali [ya wanachuoni]. Tazama dalili. Yule aliye na dalili katika waliotofautiana ndio ambaye yuko katika haki. Anayeenda kinyume na dalili haiko kwake. Tazama hili. Uko na mizani; Qur-aan na Sunnah.

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

“Mkizozana katika jambo lolote, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume.” (04:59)

Hatubaki kwenye tofauti kwa madai ya eti ya kwamba maadamu jambo hili lina tofauti hivyo tuwaache watu wabaki kwenye matamanio yao. Hapana. Ikiwa jambo lina tofauti na dalili iko na kundi moja katika hali hii unatakiwa kufuata dalili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf%204-13-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015