Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa fisi ni mnyamamkali aliyebaguliwa katika wanaofaa kuliwa?
Jibu: Ndio, fisi amevuliwa. Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu fisi. Akasema: ”Ni kitoweo.”[1]
Yule asiyetaka kula nyama ya fisi hakulazimishwa. Uamuzi uko kwake.
[1] Abu Daawuud (3801). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (3801).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
- Imechapishwa: 12/10/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Fisi halali kumwinda na kumla
Swali: Je, fisi si mmoja wa wanyama wenye meno ya kuchanja? Jibu: Lakini fisi ameelezwa kuwa amebaguliwa. Inasemekana kwamba meno yake si ya kuchanja kama ya wanyama wengine wakali. Badala yake ana jino kubwa lililo duara, ambalo hutumika kusaga chakula. Swali: Kwa hivyo inafaa kumuua fisi? Jibu: Ndio, fisi ni…
In "Aina za nyama halali na zisizo halali"
Kumuua fisi Haram
Swali: Je, ikiwa fisi atamshambulia mtu inaruhusiwa kumuua? Jibu: Ndio, fisi pia anaruhusiwa kuuawa. Ingawa fisi ni mnyama halali kuwinda, ikiwa atasababisha madhara anachukuliwa kama wanyama wengine wenye madhara na inaruhusiwa kumuua.
In "Aina za nyama halali na zisizo halali"
Damu ya fisi ni tiba inayokubalika Kishari´ah?
Swali: Je, damu ya fisi ni dawa ya baadhi ya maradhi? Nimemuona mtu anainywa na kusema kwamba ni dawa? Jibu: Damu yake ni najisi. Damu yenye kuchirizika wakati wa kuchinja haitumiwi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Allaah hakufanya kupona kwa Ummah wangu kwa yale aliyoharamisha.”
In "Damu"