Swali: Je, kuna tofauti kati ya pote lililookoka (Firqat-un-Naajiyah) na kundi lililonusuriwa (Twaaifat-ul-Mansuurah) au ni hiyo hiyo moja?
Jibu: Ni hiyo hiyo moja. Pote lililookoka ndio kundi lililonusuriwa na wao ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kama alivyobainisha hilo Abul-´Abbaas (Rahimahu Allaah) kwenye kitabu chake ´Aqiydat-ul-Waasitwiyyah. Amesema:
“Wao ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, pote lililookolewa na kundi lililonusuriwa.”
Ni Maswahabah na wale waliowafuata kwa wema. Vilevile ni wale waliomo juu ya yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Wao ni pote lililookoka, kundi lililonusuriwa na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Mwenye kutenganisha hayo hana mashiko.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/AbdelazizRajhi/Tahauiya2/01.mp3
- Imechapishwa: 06/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)