Hawa ndio wanaidhuru Salafiyyah

Swali: Ni ipi hukumu ya kujinasibisha na Da´wah Salafiyyah?

Jibu: Ni vuzuri. Unataka ajinasibishe na Da´wah za kizushi na madhehebu ya wapotevu? Ajinasibishe na Salafiyyah. Lakini iwe kihakika na isiwe kimadai tu. Lakini ni lazima ujue ni upi mfumo wa Salafiyyah ili uweze kushikamana nao. Sio uwe mwenye kudai Salafiyyah lakini hujui ni kitu gani. Kuna madhara mengi yamepatikana kwa kufanya hivi. Ni wangapi wamedai Salafiyyah ilihali hawajui ni kitu gani Salafiyyah na wameichafua Salafiyyah. Ni lazima usome mfumo wa Salafiyyah na uujue. Baada ya hapo ndio ushikamane nao. Hili ndio la wajibu.

Check Also

Sababu ya Ahl-us-Sunnah kuyaingiza mambo haya katika `Aqiydah

Hichi ni kitabu kinachoitwa “Lum´at-ul-I´tiqaad” ni katika vitabu vifupi kuhusu ´Aqiydah. Kimezungunzia masuala ya ´Aqiydah …