Ndio maana wengi walio na vyeti vya juu hawaijui Tawhiyd

Ndugu! Sote tuna haja ya kujifunza na kusoma. Hili linatuhusu sisi sote. Asiwepo yeyote atayesema kuwa ametosheka na kusoma kwa sababu eti amesoma chuo kikuu au amefikia shahada ya pili. Wengi katika wale walio na shahada za juu hutowaona wana elimu ya Tawhiyd. Kwa nini? Kwa sababu hawakujifunza elimu yenye manufaa na elimu sahihi kwa mfumo wa wema waliotangulia. Kinachotakiwa ni kuchukua elimu kutoka katika Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa Salaf. Huu ni wajibu wetu sote. Kwanza tuanze kujifunza wenyewe. Tusijisifu nafsi zetu.

Ndugu! Kutojifunza Tawhiyd ni kujisifu. Allaah ametukataza kujisifu:

فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ

“Msizitakase nafsi zenu.” (53:32)

Jifunze! Endelea kusoma! Kisikuzuie kitu na kuendelea kusoma huku kwa hali yoyote ile isipokuwa tu kwa kuwepo udhuru wa Kishari´ah ambao ni lazima uufikie. Zingatie haya.´

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Zayd al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/MouhamadBenZaydMadkhali/Divers/29.Mo7adara-16-8-1435.mp3
  • Imechapishwa: 06/09/2020