Swali: Baadhi ya vijana wanashuku juu ya uhalisi wa Fatwa kuhusiana na Salmaan al-‘Awdah na Safar al-Hawaaliy na wanasema kuwa baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa hawakusema hivo kabisa na kwamba ni uongo uliozuliwa na serikali. Je, maneno haya ni kweli?

Jibu: Madai haya yakuzuliwa yanatoka kwa viongozi wa Hizbiyyuun. Vinginevyo, wanaweza daima kwenda kwa Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz bin Baaz na kumuuliza au kumuandika mwanachama yeyote na kumuuliza. Wanapatikana.

Hizbiyyuun wanachokusudia ni kuitukana nchi kwa yote. Wanachotaka ni kusema kwamba nchi inataka kuwafunga wanachuoni kwa dhuluma, jambo ambalo ni uongo. Nchi ni adiliu na himdi zote ni Zake Allaah. Nchi haikuwafunga kwa sababu ya yanayosemwa juu yao. Walitiwa jela kwanza baada ya Kibaar-ul-´Ulamaa kujadiliana nao kuwataka wajirudi kwa waliyoyasema na kufanya. Wakakataa. Hivyo Kibar-ul-´Ulamaa wakaamua waendelee kubaki katika hali yao na wasizungumze ili kuilinda jamii. Hapa tuna Fataawaa. Wanaosema hivo wanaotamka namna hiyo wanaitukana nchi na Kibaar-ul-´Ulamaa. Ni haramu.

Yale yanayonasibishwa kwa Kibaar-ul-´Ulamaa ingelikuwa ni batili, wanachuoni wasingelinyamazia na khaswa kwa kuzingatia kuwa limetoka kwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz ambaye anasema kwa jina la wanachama wote wa kamati na anapiga muhuri mwenyewe kwenda kwa waziri wa mambo ya ndani.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah ´an al-Manaahij ad-Da´wiyyah, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 23/04/2015