Kinachosemwa juu ya Sayyid Qutwub kinaweza kusemwa pia juu ya kaka yake Muhammad Qutwub. Baada ya yote, yeye ndiye amechukua jukumu la kazi ya kueneza vitabu vya Sayyid Qutwub vitabu na kuchapisha mamia ya matoleo yake bila ya kutahadharisha kosa hata limoja yaliyomo humo. Hii ni dalili ya wazi inayoonesha kuwa anaridhia yaliyomo. Uhakika wa mambo ni kwamba, yeye anafikia hata kuvieneza. Pamoja na hivyo, Muhammad Qutwub si khatari sana kama ndugu yake. Mara nyingi anajaribu kutafsiri, kuzungunza kwa ujumla na kuepuka kuingia kwa undani. Ni mmoja katika waelekezaji wakubwa wa al-Ikhwaan al-Muslimuun. Kitabu chake “Waaqi’unaa al-Mu’aaswir” ni ushahidi bora juu ya hilo.

Baada ya kugundua Da´wah ya Hasan al-Bannaa na nguvu zake na kuenea kwake, akakosoa kasi yake kasi yake ambayo sio sehemu katika mfumo wake:

“Hatua ya kwanza ilikuwa inahusu kukusanya umati wa watu kabla ya kuwadia wakati wake.”1

Alisisitiza juu ya mafundisho ili msingi uweze uweze kuchukua sura na kusema:

“Ama kuhusu wale wanaouliza ni muda kiasi gani tutafundisha kabla ya kuanza kuchukua hatua, hatuwezi kuwapa tarehe maalum. Tunawaambia miaka kumi kutoka sasa. Hata hivyo, ni dhana tu ambazo hazikujengeka juu ya ushahidi wa wazi. Kitu tunachoweza kuwaambia kwao ni kuwa tufundishe mpaka pale ambapo lengo lililowekwa la msingi litapochukua sura ya kutosha ilio na nafuu. “2

Swali alilojiuliza mwenyewe: Unamaanisha nini na hatua? Je, mafundisho sio hatua? Ni dhahiri kwamba anazungumzia kuhusu hatua maalum – si jengine zaidi ya uasi dhidi ya serikali na wanaserikali.

(1) Waaqi’unaa al-Mu’aaswir, uk. 11.

(2) Waaqi’unaa al-Mu’aaswir, uk. 486

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Saalim as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fikr-ut-Takfiyr, uk. 176-178
  • Imechapishwa: 23/04/2015